19 Machi 2011 - 20:30

Al jazira imetangaza siku ya Ijumaa kuwa waandamanaji 2 nchini Misri wamefari katika vurugu zilizotokea baina yao na Jeshi la polisi mkoani suezi.

Madaktari wa Misri wamesema kuwa: Jeshi la polisi lilipokuwa likitawanya waandamanaji hao, ndipo polisi wakarusha risasi nakuwajeruhi waandamanaji wawili ambapo kutokana na ukubwa wa majiraha waliaga dunia, waandamanaji hao walikuwa wakikusudia kuvamia makao makuu ya Jeshi la polisi mkoani Suezi na polisi hao kuwapiga risasi.Katika hali hiyo pia watu 800 wamjeruhiwa katika vurugu baina ya waandamanaji na Jeshi la polsi mjini Cairo na  sababu ya vurugu hizo ni mauaji ya watu 74 yaliotokea baada ya mpila siku ya juma tano mkoani post saidi, hivyo basi maandamano hayo yalikuwa kwaajili ya kupinga mauaji hayo.Mauaji hayo yamewakasirisha wananchi na wabunge wengi wa nchi hiyo, na Wabunge hao walikaa kikao cha dharura na kumtuhumu waziri wa nchi hiyo kwa kuzembea.